Tetema Yafutwa Youtube Rayvanny Yamkuta Tena, Prodyuza Ahusika


 Tetema Yafutwa Youtube Rayvanny Yamkuta Tena, Prodyuza Ahusika

Rayvanny

MAJANGA bado yanamuandama msanii wa Bongo Fleva, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ baada ya video ya wimbo wake wa Tetema aliyomshirikisha aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz imefutwa kwenye chaneli ya YouTube.

 

Inaelezwa Tetema imefutwa na prodyuza maarufu Bongo anayefanya kazi kwa karibu na Lebo ya WCB, Salmin Kassim ‘S2Kizzy’ ambaye ndiye alitengeneza ngoma hiyo huku akidai kuwa anamdai Rayvanny pesa zake za kutengeneza ngoma hiyo ambayo mpaka sasa hajalipwa.

 

Tayari video hiyo ilikuwa tayari imepata views zaidi ya milioni 60 na ndiyo video iliyokuwa imetazamwa na watu wengi zaidi kwenye chaneli ya Rayvanny.


Video ya Tetema imefutwa Youtube

Ukiingia mtadao wa Youtube kwa sasa kuitafuta TETEMA iliyoachiwa rasmi mnamo Februari 7, 2019 basi utakuta audio pekee na sio video yake iliyosumbua wakati inatoka na kuibua mijadala kuwa Rayvanny alikopi na kupesti video ya ‘See You Again’ ya Tyler the Creator.

 

Tukio hili linajiri ikiwa ni miezi michache baada ya Rayvanny kujiondoa katika Lebo ya WCB na kuamua kujitegemea katika lebo yake mpya ya Next Level Music.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post