HIZI Hapa Sababu Zitakazokufanya Usiache Kula Ndizi Kamwe


 Mara kadhaa tumekuwa tukizungumza faida za matunda kiafya, lakini leo napenda tuzungumze tena kuhusu sababu hizi muhimu ambazo zitakufanya utumie ndizi kama tunda muhimu kwa afya yako.


Sababu zifuatazo zitakufanya usiache kutumia ndizi kama tunda.

Ni tunda ambalo limesheheni madini ya potassium ambayo huweza kusaidia kuweka uwiano katika kiwango cha msukumo wa damu ndani ya mwili na hivyo kulinda afya ya moyo kwa ujumla.

Aidha ndizi zinaelezwa kuwa na uwezo wa kupambana na matatizo ya kupooza yaani stroke endapo tunda hilo litatumika mara kwa mara.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la 'American Heart Association' lilieleza kuwa ndizi zinauwezo wa kupunguza tatizo la kupooza kwa asilimia 20 ikiwa tunda hilo litaliwa mara kwa mara.

Pamoja na hayo ndizi zinasifika kwa kuongeza nguvu kwa haraka ndani ya mwili, hivyo ni tunda ambalo linashauriwa kutumiwa na wanamichezo pia.

Ndizi pia huboresha mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni kwa sababu tumbo hilo lina kiwango cha fiber pia.

Mbali na hayo ndizi pia ni nzuri kwa wenye vidonda vya tumbo pamoja na matatizo ya kiungulia cha mara kwa mara.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post