Barnaba Ft. Diamond Platnumz LYRICS - Hadithi


 Barnaba  Ft. Diamond Platnumz LYRICS - Hadithi

Oooh mtume roho yangu inashindwa kuvumilia,
Si kwa mahaba anayonipa, yazidi mpaka namwagikiwa
Ananipa vinono mpaka nahisi changanyikiwa,
Hongera wake somo mtoto kafundwa katimilia
Wali kwa maini maji ya mdalasini
Na nikirudi nyumbani ananiuliza nianze chakula ama mimii
Hapo ndo ananivurugaga,
Kichwa kinaniumagaaa,
Ndo maana nimewaitaga, mnipe ushauri

CHORUS
Aaaaha Hadithi Hadithi Tamu Kolea,
Mwenzenu mimii tamu kolea,
Mchumba wangu Tamu Kolea,
Aaah sisemii, Tamu Kolea

Aaaaha Hadithi Hadithi Tamu Kolea,
Mwenzenu mimii tamu kolea,
Mchumba wangu Tamu Kolea, Basi sisemii

VERSE 2
Kanionesha jua la asubuhi,
Lavyopenya kwa dirisha na mizungu ambayo siijui amenifundisha,
Shombo la maharani amenisafisha yaya,
Kama hoi sijitambui navyojibebisha

Aaaaaah oooh, Mmmh kanitunza mahaba tamu kutaraji taa (lebe lebee)
Kibababaa michezo ya makida kida (lebe lebe)
Tunawakera waja mbona mtapata shidaa,
Niwape siri labda puto limepata mwibaa
Aaaaha eee nilonge nsilonge (longaa)
Mwenzenu mimi (longaa)
My Baby wangu (longaaa) Mi namlove

CHORUS
Hadithi Hadithi Tamu Kolea,
Mwenzenu mimii tamu kolea,
Mchumba wangu Tamu Kolea,
Basi sisemii, Tamu Kolea

Aaaaha Hadithi Hadithi Tamu Kolea,
Mwenzenu mimii tamu kolea,
Mchumba wangu Tamu Kolea Hapo Sisemi

OUTRO
Ati ona mtoto kataka nami sijivungi,
Nampa nampa tena nampa.
Nampa ale kusaza, nampa nampa tena nampa
Sibakizi hata tonee, nampa nampa tena nampa
Nampa kitu anapenda, nampa nampa tena nampa,
Nampa tamu tamuuu, nampa nampa tena nampa
Ale ajigaragaze, nampa nampa tena nampa

Next Post Previous Post