Sri Lanka Witnessing the Inauguration of a New President, He is Given Great Expectations
Rani Wickremesinghe Rais mpya wa Sri Lanka
RAIS mpya wa Sri Lanka Rani Wickremesinghe ameapishwa leo kufuatia maadamano makubwa ya umma yaliomlaazimisha mtangulizi wake kuikimbia nchi.
Kuapishwa kwa Wickremisinghe mwenye umri wa miaka 73, kumejiri siku moja baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo katika kura ya siri ilipigwa na wabunge, ambapo aliungwa mkono na chama tawala cha Sri Lanka People’s Party.
Wickremesinghe ni mmoja wa wanasiasa wenye uzoefu zaidi nchini Sri Lanka, akitokea kwenye familia ya wabunge na amewahi kuhudumu kama waziri mkuu mara sita.
Waandamanaji wa Sri Lanka waliokuwa wakitaka mabadiliko ya uongozi wa nchi hiyo
Rais huyo mpya ameahidi kuchukuwa hatua dhidi ya waandamanaji wanaofanya vurugu, lakini amesema hatoingilia kati maandamano ya amani.
Rais wa zamani Gotabya Rajapaksa alilaazimika kujiuzulu baada ya mamia kwa maelfu ya watu kuingia mitaani kupinga utawala wake. Aliikimbia nchi Julai 13 na baadaye akajiuzulu rasmi.