VIDEO: SHILOLE Haishiwi VITUKO, Anataka Kuanza FORM ONE


Mwanamitindo maarufu Bongo, MIRIAM ODEMBA, kupitia ODEMBA FOUNDATION, Agosti 27, 2019 ametembelea wilaya ya Kisarawe na kukutana na Mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo, kwa lengo la kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wilayani humo.

Katika safari hiyo, Odemba, ameongozana na mwanamuziki Shilole, ambaye amemuomba mkuu wa wilaya hiyo kumtafutia darasa ili aanze elimu ya kidato cha kwanza kwani ameishia darasa la saba tu, hivyo umefika wakati wa yeye kurudi shule kujiendeleza na elimu.

Shilole amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza historia ya Miriam Odemba, ambaye amesimulia ukweli wake kuwa hana elimu japokuwa ni mwanamitindo wa kimataifa, historia ambayo wakati anaisimulia ikamtoa Machozi DC jokate na kumgusa Shilole hadi akafikia uamuzi huo.

New VIDEO: SHILOLE Haishiwi VITUKO, Anataka Kuanza FORM ONE brand new Song Bongo Fleva recording track that has been released by the talented artist.

Next Post Previous Post